UTEUZI WA WANAFUNZI VYUO VYA AFYA


MATOKEO YA AWALI KWA
WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA VYUO VYA
AFYA
1. Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
linapenda kuwaarifu wote walioomba kujiunga na
kozi mbalimbali za afya kwa ngazi ya Cheti
(Astashahada) na Diploma (Stashahada) kupitia
Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) kuwa, Uteuzi
wa awali umefanyika na waombaji 9306 kati ya
21228 wameteuliwa kujiunga na vyuo
mbalimbali. Matokeo ya uteuzi huo yanapatikana
katika kurasa binafsi (Profiles) za waombaji.
2. Waombaji wote ambao wamechaguliwa katika
awamu hii wanapaswa kuthibitisha kuwa
wataripoti katika vyuo walivyopangiwa na
mwisho wa kuthibitidha ni Ijumaa tarehe 16
Oktoba 2015. Iwapo muombaji hatathibitisha,
nafasi hiyo itatolewa kwa mwingine. Kuweza
kuthibitisha bonyeza hapa
3. Kwa wale ambao bado hawajapangiwa vyuo,
kurasa binafsi zenu zina maelezo yenye sababu
za kutopangiwa chuo katika awamu hii na
maelekezo ambayo unatakiwa kuyatekeleza ili
mfumo utakapochakata uteuzi wa awamu
nyingine siku ya Jumatatu 19 Oktoba 2015 idadi
kubwa zaidi ya waombaji iweze kupangiwa vyuo
kwani hadi sasa nafasi zipatazo 11566
hazijajazwa.
Imetolewa na:
Katibu Mtendaji
Baraza la Taifa la Elimu yaUfundi (NACTE)
27 Septemba 2015


0 maoni: