KWAHERI KINGUNGE


Mwanasiasa Mkongwe Kingunge Ngombare Mwiru
jana ametangaza kujiondoa ndani ya Chama cha
Mapinduzi CCM na sasa atakuwa mwananchi huru.
Kingunge amezungumza jana mbele ya waandishi
wa Habari akiwa nyumbani kwake Kijitonyama, Dar
es salaam.
Amesema kutokana na matukio yaliyotokea katika
kumpata mgombea Urais kupitia chama chake ni
tofauti na ilivyokuwa mwaka 1995 na 2005 hivyo
ameamua kuondoka ndani ya chama hicho na
sasa yupo huru.
Kingune amesema hawezi kuhimili chama
kisichojiendesha bila katiba na anajua uamuzi
wake utawasumbua baadhi ya ndugu zake, wazee
na makada wengine.
Mwanasiasa huyo amesema kwa sasa hakusudii
kujiunga na chama kingine chochote kwa kuwa
amekuwa mwanaharakati kwa miaka 61.
Pia amesema yeye ni raia na ana haki zake za
kisiasa na kijamii na ataendelea kuwa na
mahusiano mazuri na nchi yake. .”Hali ya sasa
jinsi ninavyoona vijana, wafanyakazi, wakulima
wanataka mabadiliko na mimi nipo upande wa
mabadiliko kwa sababu wakati tukiwa TANU
tulifanya mabadiliko na kuunda CCM”… KINGUNGE


0 maoni: